Wito wa rais Macron wapelekea ujenzi wa kambi mbili kwa ajili ya wahamiaji mjini Calais
Serikali ya Ufaranasa baada ya wito wa rais Macron kuhusu wahamiaji, kambi mbili mpya kwa ajili ya wahamiaji Calais zitafunguliwa.
Rais Macron alisema kuwa hakati kuona wahamiaji wakiwa bila ya makaazi na kufuatilia uboreshaji wa hali za wahamiaji.
Kufuati hatua hiyo serikali ya Paris itafungua kambi mbili kwa ajili ya wahamiaji Kaskazini mwa Ufaransa katika mji wa Calais.
Waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa Gerald Collomb aliwaambia waandishi wa habari katika mkutano kuwa serikali inafuati amri iliotolewa na rais Emmanuel Macron.
Wahamiaji katika kambi hizo watakuwa wakielekezwa katika vituo vya kuomba hifadhi.
Kambi hizo zitakuwa na uwezo wa kupokea watu 300 na kutoa kiwango cha fedha kwa wahamiaji watakao amua kurejea katika mataifa.
No comments:
Post a Comment