Singida United ndiyo timu inayoonekana kuwa ni timu iliyofanya usajili wa idadi kubwa ya nyota wapya ikiwa imesajili jumla ya wachezaji 16 wapya kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Tanzania Kuu Bara.
Singida United ndiyo imepanda daraja msimu huu ikitokea Ligi Daraja la Kwanza na bahati nzuri moja kwa moja wamepata wadhamini kadhaa na imekuwa moja ya timu inayopata malezi mazuri na hivi majuzi tu ikipata basi kubwa la kisasa kwa matumizi ya kikosi hicho.
Kampuni ya Kubashiri ya SportPesa imekuwa ya kwanza kujitokeza kuidhamini Singida United kwa kutoa kitita cha Sh milioni 250 kwa mwaka huku wengine kama Puma nao wakiingia kutoa sapoti ya udhamini.
Wakati Singida United ikiwa imeanza maandalizi kwa ajili ya msimu mpya, tayari imeshaanza kuwa gumzo kutokana na kusajili wachezaji wengi wapya lakini pia ule uamuzi wa kumchukua Kocha Mholanzi Hans van Der Pluijm.
Kama utataja kocha bora ndani ya misimu minne katika Ligi Tanzania Bara, Pluijm raia wa Uholanzi ndiye kocha bora kabisa zaidi ya wengine kwa kuwa amebeba ubingwa na Yanga zaidi ya mara moja katika muda huo na kikosi chake kilionyesha uwezo mkubwa.
Hawa ndiyo wachezaji 16 ambao wamesajiliwa katika klabu ya Singida United
1. Elisha Muroiwa (Zimbabwe)
2. Twafadzwa Kutinyu (Zimbabwe)
3. Simbarashe Nhivi (Zimbabwe)
4. Wisdom Mtasa (Zimbabwe)
5. Shafik Batambuze (Uganda)
6. Dany Usengimana (Rwanda)
7. Michel Rusheshangoga (Rwanda)
WACHEZAJI WAPYA WA NDANI:
1. Atupele Green (JKT Ruvu)
2. Miraji Adam (Africa Lyon)
3. Kenny Ally (Mbeya City)
4. Roland Msonjo (Mshikamano FC)
5. Pastory Athans (Simba)
6. Deus Kaseke (Yanga)
7. Ally Mustapha ‘Barthez’ (Yanga)
8. Salum Chuku (Toto Africa)
9. Kigi Makasi (Ndanda FC)
No comments:
Post a Comment