Monday, April 9, 2018

9 APRIL 2018,TAHADHARI KWA WANYWAJI WA KAHAWA NA WASIOTUMIA

Wanasayansi wamegundua kuwa unywaji wa kahawa unasaidia mzunguko wa haraka wa damu kwa kusafisha kalsiamu katika mishipa.

Kwa mujibu wa "The Telegraph", wanasayansi kutoka Chuo Kikuu cha Brazil cha Sao Paulo wamechunguza mpango wa lishe na kiwango cha kalsiamu ya kwenye mishipa ya wafanyabiashara karibu 4,400 wa kahawa.

Kwa utafiti huo umeonyesha kuwa wanywaji wa kahawa wana kiwango kidogo cha kalsiamu katika mishipa yao na mzunguko mzuri wa damu.

Hata  hivyo wanasayansi wameonya kuwa ni vizuri kutozidisha vikombe vitatu vya kahawa kwa siku.
Utafiti huo umechapishwa katika jarida la "American Heart Association".

No comments: