Rais Dkt. John magufuli amebadili maamuzi aliyoyatoa hivi karibuni ya
kurejeshwa serikalini fedha zilizokuwa zimetolewa kwa ajili ya ujenzi
wa jengo la Halmashauri ya Bumbuli lililopo wilayani Lushoto Mkoani
Tanga.
Awali Rais Magufuli alifikia uamuzi huo baada ya viongozi wa eneo hilo kutofautiana mahali pa kujenga jengo la Halmashauri na kufanya fedha iliyotolewa na serikali kukaa bila ya kutumika kwa zaidi ya miaka miwili.
Rais Magufuli ametoa uamuzi huo katika mazungumzo yake kwa njia ya simu na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela.
Shigela ameahidi kutekeleza agizo hilo na kusema atawashughulikia wale wote watakaojaribu kukwamisha zoezi hilo kama ilivyokuwa awali.

No comments:
Post a Comment