Bashir ametoa amri hiyo wiki kadhaa baada ya idadi kubwa ya
wanaharakati wa upinzani kukamatwa wakati wa maandamano makubwa dhidi ya
serikali.
Maandamano hayo yalikuwa yameitishwa kulalamikia hali mbaya
ya kiuchumi hasa ughali wa mkate katika nchi hiyo ambapo baadhi ya
wapinzani pia walitaka serikali ya Bashir ipinduliwe.
Shirika rasmi la habari la Sudan, Suna, limesema uamuzi huo wa Bashir
unalenga kuleta amani na maelewano kwa ajili ya kuandaa mazingira
mazuri ya kufikiwa malengo ya kitaifa.
Taarifa hiyo haikusema ni
wafungwa wangapi wa kisiasa walio katika korokoro za nchi hiyo wala
haikutaja majina yao.
Wanaharakati wa upinzani wanasema kuna wafungwa 50 wa kisiasa akiwemo
mwanasiasa mashuhuri, Mohammad Mukhtar al Khatib ambaye ni kiongozi wa
chama cha kikomunisti.
Hivi karibuni chama tawala cha National Congress (NCP) kilisema kuna
mpango wa kufanya mazungumzo ya kitaifa ili kuitafutia suluhiso la
kudumu migogoro ya kisiasa nchini humo.
No comments:
Post a Comment