Monday, August 21, 2017

21 August 2017, Watu wanane wafariki katika mashambulizi Chicago Marekani

Watu wanane waripotiwa kufariki katika matukio tofauti katika jiji Chicago ambalo limepewa jina la mji mkuu wa uhalifu nchini Marekeni.

Watu wanane wamefariki na wengine 54 wamejeruhiwa mwishoni mwa Juma katika matukio tofauti.

Polisi ya kulinda usalama mjini Chicago Ijumaa imetoa ripoti kuhusu mashambulizi tofauti yaliotokea katika mji huo.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo watu wanane waliuawa na wengine 54 kujeruhiwa Kusini mwa Chicago.

Ifahamike kuwa mjini Chicago watu wapatao 422 waliuawa na wengine 2013 walijeruhiwa tangu kuanza kwa mwaka 2017.

No comments: