Spika wa Bunge la Federali la Somalia,
Mohamed Sheikh Osman Jawari, hatimaye amejiuzulu baada ya nchi hiyo ye
Pembe ya Afrika kushuhudia taharuki na mgogoro mkubwa wa kisiasa kwa
wiki kadhaa.
Wiki iliyopita, Rais Mohammed Abdullahi Farmajo wa Somalia alisimamisha kikao kingine cha Bunge kilichokusudia kujadili hoja hiyo ya kumuengua madarakani Spika wa bunge hilo.
Somalia imeshuhudia malumbano makali baina ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo Hassan Ali Khaire pamoja na kundi la wabunge wanaomuunga mkono kwa upande mmoja, na Spika wa Bunge la nchi hiyo ya Pembe ya Afrika kwa upande mwingine.

Mohamed Osman Jawari, Spika wa Bunge la Somalia anatuhumiwa na wabunge kuwa anatumia vibaya madaraka yake na kuzuia kufanyiwa marekebisho katiba ya nchi hiyo
No comments:
Post a Comment