Saturday, April 7, 2018

7 APRIL 2018,TAFITI ZAONYESHA WAISLAM NCHINI MAREKANI KUFUNGWA VIFUNGO VIREFU KULIKO WENGINE

Utafiti mpya umebainisha kuwa, watuhumiwa wa uhalifu Waislamu au wenye majina ya Kiislamu nchini Marekani wanahukumiwa vifungo virefu zaidi na habari hizo kuvaliwa njuga na vyombo vya habari, kuliko watuhumiwa wasiokuwa Waislamu.
Utafiti huo uliofanywa na shirika la kutetea haki za binadamu nchini Marekani la Institute for Social Policy and Understanding (ISPU) unaonyesha kuwa, mfumo wa sheria nchini Marekani unatoa hukumu kali zaidi dhidi ya Waislamu, ikilinganishwa na wafuasi wa dini nyingine.
Utafiti wa ISPU unasema kuwa, kwa wastani, majaji nchini Marekani wanawahukumu Waislamu vifungo mara nne zaidi ya wasiokuwa Waislamu, mbali na tukio hilo kuakisiwa na vyombo vya habari nchini humo mara saba zaidi ya wafuasi wa dini nyinginezo.

Kwa mujibu wa utafiti huo, iwapo mshukiwa Muislamu na asiyekuwa Muslamu watakamatwa kwa tuhuma za kula njama ya kutekeleza shambulizi la bomu, Muislamu atahukumiwa kifungo kizito cha miaka 20 jela huku asiyekuwa Muislamu akifungwa miaka mitano jela.

Mapema mwaka huu, Kituo cha Sheria cha Hali ya Umasikini wa Kusini nchini Marekani (Southern Poverty Law Center) kilitangaza kuwa, idadi ya makundi yanayoupiga vita Uislamu nchini Marekani imeongezeka katika kipindi cha urais wa Trump na kwamba, idadi ya makundi hayo imeongezeka kutoka makundi 101 na kufika 114.

No comments: