Raia 9 kutoka China waripotiwa kukamatwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakituhumiwa kuchimba madini Ituri bila ya kuwa na kibali.
Raia hao 9 kutoka China wamekuwa wakichimba madini bşla ya kibali Ituri tangu mwaka 2011.
Taarifa hiyo imetolewa Jumapili Mambasa Kaskazini-Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Msimamizi katika kitengo kinachohusika na migodi na uchimbaji madini Ituri Deogratias Ombalia amesema kuwa raia hao kutoka China wamekamatwa wakiwa hawana kibali kinachowaruhusu kuendesha shughuli waliokuwa wakifanya Ituri.
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ni taifa barani Afrika lenye utajiri mkubwa wa madini huku raia wake wakiwa katika hali mbaya ya umaskini.
No comments:
Post a Comment