Saturday, August 5, 2017

5 August 2017, Wabunge 82 Jordan waomba balozi wa Israel kufukuzwa

Wabunge 82 wa Jordan waomba balozi wa Israel mjini Amman afukuzwe kufuatia tukio lililopelekea watu wawili kufariki nchini Jordan.

Malalamiko hayo yalitolewa na wabunge hao kufuatia vifo vya raia wawili waliouawa na mlinzi mmoja katika jiji la Amman siku 10 zilizopita.

Malalamiko hayo yanayoomba serikali ya Amman kumfukuza balozi wa Israel yalifikishwa katika baraza la bunge siku mbili zilizopita.

Wabunge hao wameomba balozi wa Jordan mjini Tel Aviv arejeshwe nyumba na balozi wa Israel Amman aondoke nchini Jordan.

No comments: