Thursday, September 14, 2017

14 September 2017,Waziri Kalemani :Aitaka Tanesco kuwarudishia umeme wakazi 500 wa Itigi Mkoani Singida

Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt.Medard Kalemani amelitaka Shirika la Umeme nchini-Tanesco kuwarejeshea umeme takribani wananchi 500 wa Mji wa Itigi wilayani Manyoni mkoani Singida waliokatiwa umeme baada ya kukutwa na risitifekina waliojiunganishia umeme kinyemela baada ya kubainika kuwa hawana hatia.

Dkt.Kalemani ametoa agizo hilo kwenye mkutano wa hadhara alioufanya katika mji huo ambapo pia ameagiza Jeshila Polisi kumtafuta na kumtia nguvuni Meneja wa TANESCO wa mjiwa Itigi Ramadhani Rajabu anayetuhumiwa kujipatia fedha zaidiya shilingi milioni 60 kutoka kwa wananchiwa mjihuo.

No comments: